Kwa nini NIA KADI
NIA KADI ilianzishwa kwa lengo moja rahisi: kurahisisha maandalizi ya matukio yako ili yawe ya furaha na bila usumbufu.
Tunajua kuwa kuandaa tukio si jambo rahisi. Kusimamia orodha ya wageni, kufuatilia waliothibitisha kuhudhuria, kutuma vikumbusho na kuhakiki wageni mlangoni kunaweza kukuchukua muda mwingi. Badala ya kufurahia siku yako muhimu, unaweza kujikuta ukihangaika na mambo mengi.
Ndiyo maana tumeunda NIA KADI mfumo rahisi na wa kuaminika wa mialiko ya kidijitali kwa aina zote za matukio. Unaweza kutengeneza na kutuma mialiko mizuri kupitia WhatsApp au SMS, kufuatilia majibu ya wageni papo hapo, na kumpatia kila mgeni kadi yenye QR Code ya kipekee kwa ajili ya uhakiki wa haraka na salama siku ya tukio.
Iwe unaandaa harusi, send-off, birthday, graduation, kitchen party, sherehe ya familia, hafla ya kampuni, au tukio lolote maalum, NIA KADI hukusaidia kusimamia kila kitu sehemu moja.
Wewe furahia tukio lako pamoja na wageni wako, nasi tutakusaidia kusimamia mengine yote.
Pakeji Zetu
- Kutengeneza Kadi ya Mwaliko
- Kusambaza Kadi kwa Waalikwa
- Kuthibitisha Mwaliko kwa Simu (Kwa wasiothibitisha)
- Posta ya "Save the Date"
- Kukagua Kadi Siku ya Tukio
- Kutuma Ujumbe wa Shukran kwa Waalikwa
- Kutumia link ya kufuatilia maendeleo ya mialiko (Ripoti)
- 1,000 SMS
- 1,000 WhatsApp
- Kutengeneza Kadi ya Michango
- Kutengeneza Ujumbe wa Michango
- Kutuma Ujumbe kwa walengwa kwa SMS & WhatsApp
- Ripoti
- 2,000 SMS
- 2,000 WhatsApp
- Kutengeneza Kadi ya Michango
- Kutengeneza Ujumbe wa Michango
- Kutuma Ujumbe kwa walengwa kwa SMS & WhatsApp
- Ripoti
Jinsi Tunavyofanya Kazi
-
1
Tunatuma mialiko
Tunatuma mialiko ya kidijitali kupitia WhatsApp na SMS, ikiwa na maelezo yote ya tukio lako.
-
2
Fuatilia RSVP
Fuatilia majibu ya wageni papo kwa papo. Fahamu waliohakikisha kuhudhuria, waliokataa, na ambao bado hawajajibu ili uwe na idadi sahihi ya wageni kwa urahisi.
-
3
Kagua na Thibitisha Kuingia
Rahisisha ukaguzi wa wageni kwa kutumia QR Code ya kipekee. Changanua Kadi ya Kidijitali ili kuwaruhusu wageni kuingia haraka, kwa usalama, na bila kutumia karatasi.
Fanya Tukio Lako Lijalo Kuwa la Kukumbukwa
Jiunge na waandaaji wengi wanaotuamini kutengeneza, kutuma na kufuatilia mialiko mizuri ya kidijitali kwa kila sherehe.