Mialiko ya Kidijitali • Usimamizi wa Matukio +255769926865 info@niakadi.co.tz
Maswali

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Kila unachohitaji kujua kabla ya kuanza.

NIA KADI ni huduma ya kidijitali inayokusaidia kurahisisha usimamizi wa wageni kwenye tukio lako.

Kupitia NIA KADI unaweza:

  • Kutengeneza na kutuma mialiko kwa wageni

  • Kutuma mialiko kupitia WhatsApp na SMS

  • Kujua nani amethibitisha kuhudhuria

  • Kujua nani bado hajajibu

  • Kusimamia wageni siku ya tukio

  • Kutumia QR Code, Card Number na Jina kuthibitisha wageni wanapoingia

Kwa kifupi, NIA KADI inakusaidia kusimamia mialiko na wageni wako kwa urahisi, ili wewe upate muda wa kujiandaa na kufurahia tukio lako bila usumbufu.

Ni rahisi sana.

  • Tunapokea Taarifaza tukio lako

  • Tunadesign na Tunatengeneza Kadi za Mialiko

  • Tunatuma Mialiko kwa wageni wako kupitia WhatsApp au SMS na Mgeni akifungua mwaliko, ataona taarifa za tukio na anaweza kujibu kama atahudhuria au hatahudhuria.

  • Repoti - Kupitia mfumo, utaweza kuona kwa urahisi, Walio thibitisha kuhudhuria, Wasiothibitisha kuhudhuria, Wale ambao bado hawajajibu.

  • Siku ya tukio - Mgeni anapoingia, anaonyesha Kadi yake ya Kidijitali yenye QR Code, ili kuthibitisha mwaliko na kurekodi kuwa mgeni tayari ameingia.

NIA KADI inaweza kutumika kwa aina mbalimbali za matukio, kama vile: Harusi, Sherehe za kuzaliwa, Mahafali, Send-off, Kitchen Party, Hafla za kampuni, Semina, Mikutano, Sherehe mbalimbali, Matukio ya familia, na matukio mengine maalum. Iwe ni tukio dogo la familia au tukio kubwa lenye wageni wengi, NIA KADI inakusaidia kurahisisha usimamizi wa mialiko na wageni.

Wageni wanaweza kupokea mialiko yao kupitia:

📱 WhatsApp
💬 SMS

Mgeni anapofungua mwaliko, ataona taarifa muhimu za tukio pamoja na sehemu ya kuthibitisha kama atahudhuria au la.

Ndiyo.

NIA KADI inakuonyesha hali ya wageni wako kwa wakati unaohitaji.

Unaweza kuona:

Atahudhuria
Hatahudhuria
Bado hajajibu

Hii inakusaidia kujua idadi ya wageni unaotarajia na kufanya maandalizi sahihi ya tukio lako.

Mgeni akifika, anaonyesha Kadi yake ya Kidijitali yenye QR Code kwenye simu yake au Text Message na mfumo utathibitisha mwaliko wake, Baada ya kuthibitishwa, mgeni anaingia.

Ni haraka, rahisi na hupunguza usumbufu mlangoni.

Hapana.

NIA KADI inatumia mialiko ya kidijitali, hivyo mgeni anaweza kuupokea na kuuhifadhi kwenye simu yake. Hii inapunguza gharama na usumbufu wa kuchapisha na kusambaza mialiko ya karatasi.

Ndiyo.

Dashibodi yako inaweza kukuonyesha taarifa kama: Jumla ya wageni, Jumla ya mialiko, Walio thibitisha, Bado hawajajibu, Walioingia kwenye tukio, Waliobaki kuingia. Hivyo unaweza kufuatilia tukio lako kwa urahisi kabla na siku ya tukio.

Kuanza ni rahisi sana.

Wasiliana nasi kupitia simu au WhatsApp : +255769926865 na utupe maelezo ya tukio lako.

Timu yetu itakusaidia kuandaa:

Orodha ya wageni → Kadi za Kidijitali → Kutuma Mialiko → Kufuatilia Majibu → Kuingiza Wageni Siku ya Tukio

Wewe jiandae na ufurahie tukio lako. NIA KADI itakusaidia kusimamia wageni wako.

Bado Una Maswali?

Timu yetu iko tayari kukusaidia kupanga tukio lako kwa ukamilifu.